» »Unlabelled » Sadio Mane aiponza Senegal, Cameroon yatinga nusu fainali

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Brazzaville, Gabon. Timu ya Taifa ya Cameroon ‘Simba Wasiofugika’ imetinga nusu fainali ya mashindano ya Afcon baada ya kuitoa timu ya Taifa ya Senegal ‘Simba wa Teranga’ kwa jumla ya mikwaju ya penalti 5-4.
Cameroon imeungana na Burkina Fasso ambayo ilikuwa ya kwanza kutinga nusu fainali baada ya kuifunga Tunisia 2-0.
Nyota anayeichezea Liverpool, Sadio Mane ndiye aliyeiponza Senegali kwani penalti yake aliyoipiga imepanguliwa vema na kipa wa Cameroon, Fabrice Ondoa.
Dalili za Ondoa kumnyima Mane usingizi usiku huu zilionekana ndani ya dakika 90 za mchezo kwani licha ya straika huyo wa Senegal kutafuta goli, kipa huyo alilinda lango lake kikamilifu na hatimaye mchezo umemalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya 0-0.
Hata baada ya kuongezwa kwa dakika nyingine 30, Simba hao wa milima ya Teranga na Simba Wasiofugika walishindwa kufungana hadi walipoingia kwenye hatua ya mikwaju ya penalti.
Miaka 15 iliyopita, miamba hiyo ya soka ilikutana katika hatua ya fainali, Cameroon iliishinda Senegal kwa penalti 3-2 na kutwaa ubingwa wa AFCON kwa mara ya nne huko Bamako, Mali.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post