

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa
alisema hayo jana alipokuwa anahutubia wahitimu kwenye mahafali ya 32 ya
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
“Naomba kwa sasa msiniulize ni mkandarasi gani atasaini ila wakati
ukifika kila kitu kitakuwa hadharani, reli hii haitatumia gari moshi ni
umeme,” alisema Profesa Mbarawa.
Alisema reli hiyo itakuwa na mwendokasi wa kilometa 160 kwa saa.
Januari 26 mwaka huu, Rais John Magufuli alipokuwa anazindua mradi wa
magari yaendayo haraka (BRT) maarufu kama mwendokasi alisema Serikali
inapitia zabuni ili kumpata mkandarasi atakayejenga reli hiyo yenye
urefu wa kilometa 200.
