» »Unlabelled » Madini mapya yafungua ajira kwa vijana 250

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Lindi.  Zaidi ya vijana  250  wa mikoa ya Lindi  na  Mtwara, wanatarajia  kupata  ajira  baada madini  aina ya Bunyu (Kinywe) kugundulika katika  vijiji  vya Namangale, Utimbe, Chidya na Chiwata.

Hayo yameelezwa na Mhandisi wa Migodi Kanda ya Kusini, Aidan Mhando kwenye kongangamano la  wadau wa mradi wa uchimbaji wa madini ya bunyu katika vijiji hivyo.

Mhandisi Mhando alisema uchimbaji unatarajia  kuanza hivi karibuni na kwamba, hatua iliyobaki ni kupata  leseni ya uchimbaji baada ya shughuli zingine kukamilika.

Baadhi ya kampuni za utafiti zilizogundua madini hayo ni Urinex Ruangwa, Nachi Jumbo na Ngwena. Akiba ya madini hayo ambayo yana rangi nyeusi yanayotumika kutengenezea vifaa vya umeme, ni tani 689.7 milioni.

Akizungumza kwenye kongamano hilo, Mwakilishi wa  Kampuni ya Nachi Jumbo, Mhandisi Jimmy Ijumba alisema kampuni hiyo ambayo itachimba madini hayo inatarajia kusafirisha tani 100,000 hadi 180,000 kwa mwaka.

Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Selemani Mzee alitoa wito kwa wawekezaji ikiwamo Kampuni ya Nachi Jumbo kutumia uzoefu wa utekelezaji miradi iliyofanyika ili kuepuka migogoro kutokana na kutolipa fidia wananchi kwa wakati.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post