» »Unlabelled » Bana matumizi yaathiri utendaji wa Mahakama

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Moshi. Utaratibu wa kubana matumizi nchini unaonekana kuutikisa mhimili wa Mahakama, baada ya kesi za mauaji kushindwa kuendeshwa nje ya mji wa Moshi.

Mwaka jana, vikao vya kesi za mauaji vilikuwa vifanyikie wilayani Rombo kati ya Novemba 14 na Desemba, Hai ilikuwa Septemba 26 hadi Oktoba 20 na Same kati ya Mei 23 na Juni 24.

Hata hivyo, vikao hivyo havikufanyika kutokana na ufinyu wa bajeti unaoukabili mhimili huo, huku kukiwa na dalili hali hiyo kujirudia mwaka huu.

Habari za uhakika kutoka kwa mawakili wa kujitegemea, zimeeleza kuwa hali hiyo imechangiwa na Serikali kuipa Mahakama fedha kidogo kulingana na bajeti halisi.

Wakili Youngsaviour Msuya alisema licha ya Serikali kuwa na vipaumbele vyake, mhimili wa Mahakama ni muhimu katika kusimamia utulivu wa nchi.

Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) tawi la Moshi, David Shilatu alisema taarifa walizonazo ni kuwa Mahakama haina fedha za kutosha kujiendesha kwa ufanisi.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, Bernard Mpepo alikiri kuwapo kwa tatizo la fedha na kwamba, hilo limewasababisha kuendesha kesi zote za mauaji Moshi.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post