» »Unlabelled » CCM yavuna wanachama 200 waliokimbia Chadema

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Bumbuli. Wanachama 200 wakiwamo  viongozi  wa Chadema katika Kitongoji cha Kwemghogho wilayani hapa wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM .

Akizungumza baada ya  kuwapokea wanachama hao jana, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba alisema uamuzi wao unatokana na CCM kutekeleza ahadi nyingi za maendeleo.

Makamba alisema CCM imefanya  mengi  hivyo  haoni  ajabu  kuwapokea wanachama kutoka  vyama  vingine  vya siasa.

Alisema chama hicho kina kazi kubwa ya kuleta maendeleo ambayo yanahitaji umoja na mshikamano na siyo migogoro, fitina na  majungu.

Makamba alisema moja ya mambo yanayochangia kurudisha nyuma maendeleo ni baadhi ya watu kukaa vijiweni na kurushiana maneno, lakini kwa wana-CCM muda huo sasa haupo.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa  Chadema wa Kitongoji cha Kwemghogho, Shabani Kahema  aliwahamasisha vijana kujiunga na CCM kwa kuwa ilani  yake inatekelezeka  kwa  wakati.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post