» »Unlabelled » Mzee Mwinyi aonya uvunjifu wa amani

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Ikungi. Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka Watanzania wasiruhusu upungufu wa ubinadamu kuwa chanzo cha  kuhatarisha amani na utulivu unaotamalaki nchini.

Mzee Mwinyi alitoa wito huo  mwishoni mwa wiki iliyopita wakati ufunguzi wa Msikiti  Qadiriyya katika Kijiji cha Ititi, Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambao umegharimu Sh54 milioni.

Alisema Mungu ameumba binadamu ambao siyo malaika, hivyo kuhitilafiana ni jambo la kawaida na haliepukiki.

“Hatuwezi kuzikubali hitilafu hizi, lakini hatuwezi kuzikataa kwa sababu zitakuwapo tu upende usipende. Tunachopaswa kufanya ni kutoziruhusu kutumiliki, binadamu ndiyo tuzimiki. Kwa njia hiyo amani na utulivu utaendelea kudumu nchini,” alisema.

Alisema ili hitilafu hizo zisisababishe ugomvi au vurugu zitakazochangia kutoweka kwa amani na utulivu, Watanzania wanatakiwa kupendana kwa dhati na kuvumiliana. “Inapotokea bahati mbaya tukahitalifiana, isiwe sababu ya kugombana… hitilafu husika itafutiwe ufumbuzi kwa amani. Kwa ujumla kila mtu ashike yake yaliyo halali yakiwamo ya dini, ugomvi wa nini?” alihoji Mzee Mwinyi.

Alisisitiza kwamba Watanzania waendelee kudumisha utamaduni kwa kuombana radhi zinapobainika dalili ugomvi, au hitilafu.

Akitoa salamu zake, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Rehema Nchimbi aliahidi Serikali kuendelea kushirikiana kwa ukaribu na  dini zote katika kuhudumia wananchi kwa ajili ya maendeleo.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post