Monday, December 12, 2016
Moshi. Baadhi ya maofisa Uhamiaji mkoani Kilimanjaro, wanadaiwa kuwageuza raia wa kigeni wasio na vibali vya kufanya kazi kuwa mradi wa kujiingizia kipato.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini maeneo yaliyogeuzwa mradi ni shule za mchepuo wa Kiingereza zenye walimu kutoka nchini Kenya.
Maofisa hao pia wanadaiwa kuchukua rushwa kuruhusu wageni wasio na vibali kufanya kazi za Watanzania katika baadhi ya viwanda mkoani hapa.
Baadhi ya tuhuma zimefikishwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na tayari maofisa kadhaa wa idara hiyo wamehojiwa na wanachunguzwa.