» »Unlabelled » Wasichana wadogo watekeleza shambulio sokoni Nigeria

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Monday, December 12, 2016

Watoto wasichana waliotekeleza shambulio walikuwa na umri wa miaka saba na minane

Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa wasichana wawili wamelipua mabomu mawili katika soko lililoko kwenye jimbo la Borno na kumuua takriban mtu mmoja.

Mwanamgambo mmoja katika mji wa Maiduguri amesema kuwa watoto wasichana hao ambao pia waliuawa walikuwa na umri wa miaka saba na minane.

Alisema kuwa aliwaona wakitoka nje ya Bajaji na kujaribu kuzungumza na mmoja wao, ambaye baadae alielekea kwenye jengo lenye maduka mengi na kulipua vilipuzi.

Hakuna aliedai kuhusika na shambulio hilo, lakini waandishi wa BBC wanasema kundi la Boko Haram mara kwa mara hutumia wanawake na watoto katika mashambulio yake ya mabomu.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post