» »Unlabelled » Waziri Kairuki atembelea uandikishwaji wa vitambulisho vya Taifa kwa watumishi wa umma Wilayani Misungwi

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe,Angela Kairuki  akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, Eliurd Mwaiteleke mara  baada ya kuwasili katika Ziara ya kikazi mapema hii leo Wilayani Misungwi kwa lengo la kufuatilia zoezi la Uandikishaji wa Watumishi wa Umma kwa ajili ya kutoa Vitambulisho vya Taifa, zoezi ambalo limeanza tarehe 3 Oktoba, 2016 na linatarajiwa kukamilika tarehe 17,Oktoba 2016.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke kuhusu utekelezaji wa zoezi hilo, alieleza kwamba linafanyika katika Vituo viwili vya Makao Makuu Misungwi na Kituo cha Walimu Usagara na hadi sasa Uandikishaji umefanyika kwa asilimia 49. Picha na Thomas Lutego, Afisa Habari na Mawasiliano wa Halmashauri.


Mhe,Angela Kairuki Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais akishuhudia na kupewa maelezo kuhusu zoezi la Uandikishaji na Mtaalamu wa NIDA Ndg Abassi alipotembelea kituo cha Makao Makuu ya Wilaya Misungwi.

Aliyekaa kwenye kiti ni Robert Joseph Kubebeka Mwalimu wa Sekondari Misungwi akitoa taarifa Muhimu kwa ajili ya Kitambulisho cha Uraia cha Taifa.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post