» »Unlabelled » Nyumba ya muuaji wa msichana wa Kiisraeli yabomolewa

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Nyumba ya msichana wa Kiisraeli aliyeuawa na mwanamume wa Kipalestina

Jeshi la Israel linasema kuwa limeharibu nyumba ya raia wa Kipalestina aliyemdunga kisu na kumuua msichana wa Iiisraeli chumbani mwake.

Jeshi hilo limesema kuwa Mohammed Nasser Tarayrah alivunja na kuingia katika nyumba iliopo katika makaazi ya Kiryat Arba mnamo mwezi Juni na kumshambulia msichana huyo mwenye umri wa miaka 13 Hallel Yaff Ariel alipokuwa akilala kabla ya kuuawa na mlinzi wa makaazi hayo.

Sera ya Israel ya kuziharibu nyumba za raia wa Palestina wanaofanya mashambulio imekosolewa na wengi kama adhabu ya jumla.

Serikali ya Israel inasema kuwa hatua hiyo inawazuia wengine ambao wangependelea kutekeleza kitendo kama hicho.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post