» »Unlabelled » Matunzo ya mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Na James Timber

Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ni nani?
Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ni yule ambaye amezaliwa na mwanamke ambaye hajafunga ndoa na mwanaume aliyezaa naye.

Aidha kama mwanamke  ambaye ameolewa lakini anakaa mbali na na mume wake, akizaa na mwanaume mwingine mtoto atakayezaliwa atahesabiwa kuwa ni mtoto wanje ya ndoa.
Vilevile mjane akijifungua mtoto ambaye si ya marehemu mume wake atahesabiwa kuwa ni mtoto wan je ya ndoa.

Watoto wanaozaliwa katika mazingira haya matunzo yao yanasimamiwa na sheria ya matunzo ya watoto wa nje ya ndoa Sura 278 ya mwaka 1964.

Kufuatana na sheria tajwa hapo juu, mama wa mtoto huyo anaweza kupeleka maombi mahakamani akiomba mahakama imtangaze mwanaume fulani kuwa baba halali wa mtoto.

Matunzo ya mtoto, baada ya baba wa mtoto kutangazwa au kuthibitishwa na mahakama, na mama wa mtoto kuomba atoe matunzo au gharama za elimu ya mtoto na baba akikataa au kutoa kiasi cha fedha ambazo hazitoshi.

Mahakama baada ya kupokea maombi  inaweza kumwita baba huyo na kutoa amri kuwa atoe gharama za matunzo kwa mama kwa mama wa mtoto au mlezi kulingana na kipato chake.

Maombi haya yatapelekwa katika mahakama ya Wilaya kwa kuwasilisha hati ya maombi ikiambatana na hati ya kiapo.

Endapo amri ya matunzo na gharama za elimu zinatafutwa mahakamani na mama wa mtoto, itakuwa ni kosa kwa mtoto huyo kuondolewa chini ya malezi ya mama yake.

Iwapo mtu yeyote atakiuka amri ya mahakama inayotaka malezi kuwa chini ya ya mama na inayokataza kumchukua mtoto anayelelewa na mama yake mzazi.

Mtu huyo anaweza kushitakiwa na akipatikana na hatia anaweza kufungwa.
Matunzo ya mtoto yanapotolewa inabidi yatumike kwa kumtunza mtoto na wala si vinginevyo, na mtu anayefuja fedha za mtoto anaweza kushitakiwa na akipatikana na hatia anaweza kufungwa jela.

Angalizo, endapo wakati wa kupeleka maombi mahakamani, mwombaji akiolewa au kama mwombaji alikuwa ni mwanamke aliyeolewa lakini akiishi mbali na mumewe, na katika kipindi cha maombi amerudiana na kuishi na mumewe mahakama haitaweza kutoa amri ya matunzo kwa mtoto husika.

Fedha zote kwa ajili ya matunzo ya mtoto zinaweza kulipwa kwa mama au mlezi wa mtoto. Hata hivyo fedha zinaweza kulipwa mahakamani na baadaye mahakama kuzituma kwa mama au mlezi wa mtoto.

Uteuzi wa mlezi, baada ya mama wa mtoto kutakiwa kulipwa  matunzo na ikaonekana kuwa mama wa mtoto hawezi kumlea mtoto, mahakama inaweza kumteua mtu mwingine kwa ajili ya kumlea mtoto kama mtu huyo amekubaliana na uteuzi huo kwa hiari yake mwenyewe.

Baadhi ya vigezo vinavyosababisha mlezi kuteuliwa ni mama kufariki, kutokuwa na akili timamu au kufungwa gerezani.

Maombi ya kuteuliwa mlezi yanaweza kuwasilishwa mahakamani na baba wa mtoto, mama wa mtoto au Afisa Ustawi wa Jamii.

Hata hivyo baba wa mtoto anaweza kupeleka maombi kuomba mtoto husika awe chini ya uangalizi pale mtoto anapotimiza umri wa miaka saba.

By James Timber 
charitytimberland@gmail.com
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post