» »Unlabelled » Wafanyakazi 10 wasimamishwa kazi Wilaya ya Kilosa

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Morogoro. Kasi ya utumbuaji majipu kwa watumishi wa Serikali imeendelea baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Kessy Mkambala kuwasimamisha kazi watumishi 10 kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ubadhirifu wa fedha na ukiukwaji wa kanuni za uwajibikaji kazi.

Akizungumza na Mwananchi wilayani Kilosa, Mkambala alisema watumishi hao amewasimamisha kazi kwa kutokufuata kanuni na sheria mbalimbali za kiutendaji na hivyo kuisababishia hasara serikali.

Mkambala amesema kati ya watumishi hao waliosimamishwa kazi yupo mkuu wa idara ya manunuzi ya halmashauri hiyo, Geofrey Njovu kwa madai ya kufanya manunuzi yasiyofuata taratibu na kuisababishia halmashauri hasara ya mamilioni ya fedha.

Hata hivyo, Njovu alisema ni vyema Takukuru ikahusishwa kuchunguza tuhuma zinazomkabili kwani hazina ukweli wowote.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post