Katika maandalizi ya kuelekea katika mchezo wake wa tatu dhidi ya Medeama, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Yanga Juma Mwambusi amesema wanaendelea kuwajenga wachezaji kisaikolojia ili kuweza kufanya vizuri katika mchezo huo.
Mwambusi amesema mara baada ya kupoteza mchezo dhidi ya TP Mazembe wachezaji hawakuwa katika hali ya kawaida lakini wameendelea kuwaweka sawa kisaikolojia kwa ajili ya maandalizi ya kupambana na Medeama ili kuhakikisha wanakuwa katika nafasi nzuri katika hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mwambusi amesema, kila mchezaji amaendelea kuonyesha hali ya kujiamini katika mazoezi hatua ambayo ambayo inaonyesha ni nzuri kwa ajili ya mpambano wa mchezo wao wa tatu.
Mwambusi amewataka mashabiki na watanzania kwa ujumla kuwa na uvumilivu kwani hata mafanikio katika klabu hayaji kwa mara moja bali ni kujipanga kwa ajili ya kutafuta mafanikio.
Yanga ambayo ipo kundi A itashuka dimbani kupambana na Medeama Julai 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku ikiwa na rekodi mbaya ya kupoteza michezo yake miwili ikiwa ni ule wa awali dhidi ya Mo Bejaia uliopigwa Juni 19 nchini Algeria ambapo Yanga ilichapwa bao 1-0 pamoja na ule dhidi ya TP Mazembe uliopigwa Juni 28 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.