Sio Mustafa Hassanal pekee ambaye amekuwa akifanya uzinduzi wa kazi zake nje ya nchi, bali hata kwenye upande wa sanaa ya muziki wa kizazi kipya wameshuhudiwa wasanii kadhaa wakifanya hivyo hasa nchini Afrika Kusini.
Mbunifu huyo wa mavazi ameeleza wazi sababu inayowafanya kila wanapotaka kufanya uzinduzi wa mavazi wanakwenda kufanyia Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa Mustafa Hassanali amesema sababu kubwa ni wigo wa kujitangaza, kwa maana ya kwamba ukifanyia uzinduzi Tanzania utalazimika kuwekeza nguvu kubwa kwenye vyombo vya habari nakama hutafanya hivyo basi hutajulikana kama umefanya chochote.
Lakini nchini Afrika Kusini mbunifu huyo amesema unapofanya uzinduzi wako inakuwa rahisi kujulikana na kuuza kiurahisi kwa kile alichodai kuwa nchini Afrika Kusini vinapatikana takribani vyombo vyote vya habari vikubwa duniani.