Mjane mwenye umri wa miaka 66 mkazi wa kijiji cha Madisa wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma Bi Dawa Kilala pamoja na familia yake ya watoto saba wameiomba serikali iwasaidie kurudishwa kwenye nyumba yake na mifugo pamoja na mashamba yanayedaiwa chukuliwa na ndugu wa mumewe baada ya mume wake kufariki dunia.
Akizungumza na ITV ilifika kijiji hapo Bi Dawa amesema wameishi na mumewe kwa zaidi ya miaka hamsini na kujaliwa kupata nyumba na mashamba lakini baada ya mumwe Athumani Kiluta kufariki mwaka 2015 ndugu wameanza chukua nyumba na mali zingine na kumtaka aondoke akiwa na watoto saba aliyeachiwa na mke mwenzake aliyekimbia nyumbani hapo.
Majirani wamesema wanasikitishwa na kitendo cha mjane huyo kuzulumiwa mali zake kwani wanamtambua kwa muda mrefu na amehusika kwa kiasi kikubwa kuchuma mali huku mwenyekiti wa kijiji cha Madisa Juma Mohamed amekiri kumtambua mgogoro huo.
Msemaji wa ukoo wa mzee Athumani Kiluta Bwana Mohamed Kiluta amesema tukio ilo lipo lakini ugawaji umefanyika kisheria kwa taratibu za dini na majane alikubali mgao hivyo wanashangaa kwanini analalamika.