» » Magenge ya serikali yanabaka wanawake Burundi-HRW

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

 Shirika la kutetea haki za binaadamu lenye makao yake nchini Marekani, Human Rights Watch linasema wafuasi wa tawi la vijana katika chama tawala nchini Burundi wamekuwa wakiwabaka wanawake wa wale wanaoshukiwa kuwa tekeleza ubakaji wa magenge .

Ripoti hiyo inaeleza kuwa jamaa za watu walioonekana kuwa wanaunga mkono upinzani ndio waliolengwa zaidi akiwemo mtoto wa miaka minane.

Wengine wanaarifiwa kubakwa kuwatishia kutokimbia katika nchi jirani.

Kumeshuhudiwa ghasia Burundi tangu rais Pierre Nkuruziza kuamua kuwania muhula wa tatu kama rais.

Katika kisa kimoja msichana wa miaka minane anadaiwa alibakwa na genge la vijana wa kiume wanane ambao ni wanachama vuguvugu hilo hapo mwezi Aprili mwaka uliopita.

 Wengine walifungwa na kuchapwa, huku wakibakwa mbele ya jamaa na watoto wao.
Walitishiwa kuuawa endapo wangejaribu kukataa.

Waathiriwa wengi wamewataja washambuliaji hao kama wanachama wa vuguvugu la vijana ambalo awali lililaumiwa kwa kutekeleza mauaji, kuwapiga na kuwatisha wafuasi wa upinzani.

Maafisa wa polisi au watu waliovalia sare za polisi wamelaumiwa kwa kutekeleza ubakaji.

Baadhi ya wakimbizi waliokimbilia nchi jirani ya Tanzania wamedai kubakwa wakati wakijaribu kutoroka nchi, wengine wakisema walidhululiwa ndani ya kambi.

Ripoti inasema wanawake wengi walioathiriwa hawajapokea msaada wowote wa dharura na hivyo kuwaacha wakiwa na mfadhaiko.

Burundi imeshuhudia ongezeko la machafuko tangu Rais Nkurunziza kutangaza mwaka uliopita kwamba atawania muhula wa tatu uliozua utata.

Muungano wa Afrika ulifadhili mazungumzo ya amani ya Burundi, katika nchi jirani ya Tanzania, lakini mazungumzo hayo yalisambaratika.

Aidha serikali ya Burundi imepinga kutumwa kwa waangalizi wa kimataifa ambao walipitishwa na baraza la usalama la umoja wa Mataifa.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post