» » Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaanza kuhakiki idadi ya wafanyaakzi wake.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha inakuwa na ufanisi na utendaji bora imeanza mchakato wa kuangalia mahitaji halisi ya wafanyakazi wake serikalini ambao kwa sasa inawafanyakazi 40,000.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa fedha na mipango wa Zanzibar Dr Khalid Mohamed wakati akiongea na wafanyakazi wa taasisi ya uhakiki mali na rasilamli za serikali akiwa katika ziara yake ya kuangalia taasisi zilzondani ya wizara yake ambapo amesema zoezi hilo lipo na linaendelea ingawa bado hapajapatikana sababu nzito ya kusema kuwa idadi hiyo ni kubwa.

Kwa upande mwengine Dr Khalid amewaonyoshea kidole wafanyakazi wa serikali ambao wanaacha majukumu yao waliyopewa na kujitajirisha wao na kuzipinda sheria za kazi, serikali haitokubali na itahakiksha sheria dhidi yao zinachukuliwa huku akitaka taasisi hiyo ya uhakiki mali na rasilamli za serikali kufanya kazi zao kisheria kuhusu umilikaji na uuzaji wa mali za serikali.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post