» » Watuhumiwa 16 mahakamani kwa kutumia barabara za magari yaendayo haraka kinyume cha sheria

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Jumla ya watuhumiwa kumi na sita leo wamefikishwa mahakama ya mwanzo wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam, kwa kosa la kuvunja sheria za barabarani kubwa zaidi ni kutumia barabara za magari yaendayo haraka kinyume cha sheria.

Aidha kundi lingine la watuhumiwa wenye makosa kama hayo limerudishwa rumande, kufuatia taratibu za kesi zao kutokamilika, huku wengi wao wakiwa ni madereva wa magari, pikipiki, mabasi ya abiri na bajaji.

Kamera ya Channel ten ilifika mahakama ya mwanzo ya wilaya ya kinondoni na kunasa watuhumiwa kumi na sita wakipelekwa mahakamani  hapo , wengi wao wakiwa vijana, huku ndugu jamaa na marafiki wakihaha namna ya kupata utaratibu mzima wa kuweza kuwawekea dhamana ndugu zao.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyopatikana mahakamani hapo kutoka kwa ndugu za watuhumiwa wengi wa watuhumiwa hao ,wamekamatwa kuanzia tarehe tatu wiki iliyopita.

Hadi channel ten inaondoka mahakamani hapo watuhumiwa walikuwa bado hawajasomewa mashtaka yao, ingawa inadawa kuwa, kutokana na makosa waliyotenda , wanaweza kupewa adhabu ya kutozwa faini au kifungo au vyote.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post