» » Naibu Spika asema ipo haja ya kurekebisha kanuni za bunge ili kuwabana wanaosusia vikao.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Naibu  Spika  wa  bunge la Jamhuri Muungano  wa Tanzania  Mh  Dk.  Tulia Ackson  amesema   ipo  haja ya kurekebisha  sheria  na  kanuni   za  uendesaji wa bunge   kwa  lengo  la kuhakikisha   kuwa  kila  mbunge   analipwa   posho  baada   ya  kutekeleza   majukumu  yake   ipasavyo   na  siyo  kujisajili  kwa lengo  la  kupata  posho   na  kisha  kutoka   nje  bila   ya  kutekeleza  majukumu   yake   ya   kikatiba.

Mh .Tulia   ameyasema  hayo  alipokuwa   akitolea  ufafanuzi  miongozomiwili iliyowasilishwa  bungeni  hapo  na  baadhi   ya  wabunge  akiwemo  Mh  Dk. Harison  Mwakyembe   ambaye  ni waziri wa katiba na sheria   aliyetaka  kujua  uhalali  wa wabunge wa upinzani kuendelea  kulipwa posho na mishahra wakati kila   kikao kikiongozwa na   Naibu  Spika  wamekuwa  wakitoka nje.

Pendekezo hilo la Naibu Spika la kurekebishwa kwa sheria linaungwa mkono na mbunge wa Mkuranga Mh.  Abdalah   Ulega  ambaye  anasema  ni  vyema sheria  zibadilishwe  ili kurudisha  heshima  kwa  kiti   kwani   kitendo kinachofanywa  na wapinzani  kwa siyo  cha  kiungwana.

Peter  Msingwa  ni  mbunge  kutoka  Chama  Cha  Demokrasia  na maendeleo  CHADEMA ambaye   anasema  bunge  linaongozwa  kwa  misingi  ya sheria  na kanuni  na  siyo  kweli kuwa  mbunge  katika kutekeleza  majukumu yake  ni  lazima  aingie  bungeni  zipo  kazi nyingi  za  kibunge  zinafanyika nje  ya ukumbi  wa   bunge.

Awali  katika   kipindi  cha  maswali  na  majibu  mawaziri na  manaibu  mawaziri walipata nafasi  ya   kujibu  maswali mbalimbali  ya  wabunge  ambapo  maswali ya  wabunge kutoka  kambi   upinzani  yaliulizwa na wabunge wa  CCM  ambapo masuala  kama changamoto   za   maji  majimboni   hayakukosekana.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post