Maelezo ya awali ya Kesi inayowakabili watu watatu akiwemo raia wa China Feng Glan,maarufu malikia wa Tembo, wa kusafirisha nje ya nchi meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5.4, leo yameshindwa kutolewa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam,kufuatia Mkurugenzi wa mashitaka nchini kutoa maelekezo ya kukamilishwa kwa upelelezi katika baadhi ya maeneo.
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Huruni Shahidi,wakili mkuu wa Serikali ambae anaiwakilisha jamhuri katika kesi hiyo,amesema mkurugenzi mkuu wa mashtaka DPP amelipitia shauri hilo na amelizika ila ametoa maelekezo ya kufanyia upelelezi katika maeneo kadhaa katika shauri hilo.
Wakili mkuu huyo amesema,maelekezo ya DPP ni yakawaida kwenye mchakato mzima wa kiupelelezi ambapo ameeleza matumaini yake kuwa upelelezi huo utakamilishwa haraka iwezekanavyo ili shauri hilo liende katika hatua inayofuata ambayo ni ya usikilizwaji.
Kutokana na maelekezo hayo ya DPP,Kesi hiyo,ambayo Watuhumiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari Mosi mwaka 2000 na Mei 22 2014 jijini Dar es Salaam, ambapo kwa pamoja inadaiwa walijihusisha na vipande 706 vya meno ya tembo vyenye thamani ya shilingi bilion 5.4, itatajwa tena Juni 20 kwa ajili ya washitakiwa kusomwa maelezo ya awali ya kosa lao.
Watuhumiwa wataendelea kukaa mahabusu kufutia DPP kuzuia dhamana na kuridhiwa na mahakama kuu kufutia tuhuma dhidi yao kuangukia katika makosa ya uhujumu uchumi,ambayo sheria inakataza dhamana kwa shtaka linalozidi milioni kumi.