» » Mbinu Mpya ya kuwakamata wafanyabiashara wakubwa wanaonunua nyara kutoka kwa majangiri

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Kufuatia serikali kutumia nguvu kubwa katika mkupambana na majangiri huku changamoto hiyo ikionekana kuwa bado ni kubwa, serikali  imeanza kutumia mbinu mpya ya kuwakamata wafanyabiashara wakubwa wanaonunua nyara kutoka kwa majangiri ili kukomesha kabisa vitendo hivyo.

Waziri wa maliasili na utalii Prof Jumanne Maghembe, amesema hayo wakati akiongea na waandishi wandamizi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni njia moja wapo ya kuongeza mawasiliano kati ya tanapa na vyombo vya habari ambapo amesema mpaka sasa tayari wameshakamata watuhumiwa sita wanaonunua nyara hizo huku wengine nane wakiwa wanatafutwa.

Kwa upande wake meneja mahusiano wa hifadhi za taifa TANAPA Paschal Sherutete amesema ipo haja kwa jamii zinazozunguka  hifadhi mbalimbali za taifa kuwa makini na kulinda hifadhi hizo kutokana na uharibifu unaofanyika ukiendelea  unaweza kusababisha madhara kwa taifa kwa kukosekana kwa ajiri kwa zaidi ya watu milioni mbili huku mhariri mtendaji wa New Habari 2006, Abdisalum Kibanda ameiomba serikali kuongeza kunguvu katika jitihada za kuongeza watalii kwa kutumia fulsa zinazojitokeza katika mataifa mbalimbali duniani.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post