Mamlaka ya mapato Tanzania TRA kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya mapato imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 1.032 katika mwezi mei mwaka huu ambayo ni sawa na asilimia 100.7 ikiwa ni juhudi zilizowzesha kupita lengo lililokusudiwa la kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 1.025 kufikia mwezi huo.
Kamishna mkuu wa TRA Bw Alphayo Kidata ametoa taarifa hiyo alipokuwa akizunguimza na waandishi wa habari mjini Moshi kuhusu ambapo amesema tra itaendelea na jitihada za kuhakikisha inavuka lengo lililowekwa na serikakali kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 kwa kukabiliana na vikwazo vinavo kwamisha ukusanyaji wa mapato.
Aidha Bw Kidata amesema tra katika kuhakikisha wafanyabiashara wanatoa ushirikiano katika matumizi ya mashine za EFD wameanza kugawa mashine hizo kwa wafanyabiashara wadogo kwa mkoa wa Dare salaam na kuongeza kuwa, zoezi hilo litaendelea katika mikoa yote ya Tanzania kwa utaratibu maalumu uliyowekwa.
Zoezi la matumizi ya mashine za EFD litasaidia kuongeza mapato ya serikali kwa ushirikiano wa wafanyabiashara na wananchi sambamba na kutoa taarifa kwa mamlaka ya mapato kuhusu wafanyabiashara wote watakaokiuka kutumia mashine hizo.