Mahakama ya Kisutu.
Dar es Salaam.
Mawakili wa Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na wenzake watatu
katika kesi ya uchochezi iliyofunguliwa jana katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wamepinga korti hiyo kusikiliza shauri hilo
kwa madai haina mamlaka kisheria.
Mkina
na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uchochezi baada ya kuandika na
kuchapisha makala yenye kichwa cha habari “Machafuko yaja Zanzibar”
katika gazeti la Mawio la Januari 14-20, mwaka huu.
Washtakiwa
wengine katika kesi hiyo, mbali na Mkina, ni mwandishi wa makala hiyo,
Jabir Idrissa ambaye ni mshtakiwa wa kwanza; Ismail Mehboob, ambaye ni
mmiliki wa mtambo uliochapisha gazeti lenye makala hiyo, na Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu.
