» »Unlabelled » Lukuvi ataka vijiji vyote vipimwe ifikapo 2025

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameitaka Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ili kufikia mwaka 2025 vijiji vyote viwe vimesimamiwa, vimepimwa na kumilikishwa kwa wanavijiji.

Lukuvi ameyazungumza hayo leo wakati akizindua Kamisheni hiyo na kusisitiza kuwa Tume hiyo imeundwa kwa mujibu wa matakwa ya Fungu la 6 la sheria ya Upangaji wa Matumizi ya Ardhi no. 6 ya mwaka 2007 na inajumuisha wajumbe kutoka sekta za Umma, Sekta binafsi na sekta za kijamii.

"Majukumu yenu ni kusimamia uendeshaji wa shughuli za tume, kuratibu shughuli za taasisi zote zinazohusika na shughuli za Upangaji wa matumizi ya ardhi na kuwa kiungo cha mawasiliano cha Taasisi hizo za Serikali lakini pia kumshauri Waziri wa Ardhi kuhusu masuala yote yanayohusu mipango ya matumizi ya ardhi," amesema Lukuvi.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post