Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu amesema Taifa lina uhaba mkubwa wa damu salama lakini wananchi
hawana mwamko wa kuchangia damu kwa kuwa wanapochangia hutakiwa kununua
damu hiyo.
Akizungumza
jana kwenye maadhimisho ya kuchangia damu salama yaliyofanyika kitaifa
kwenye uwanja wa Nyerere square Mwalimu amesema kuwa tabia ya waganga
Wakuu wa Hospitali za Wilaya na Mikoa kuwauzia damu wagonjwa ndiyo
chanzo cha wananchi kutokuwa na moyo wa kuchangia damu.
Amesema
wananchi wamekuwa wakikatishwa tamaa na madaktari pale wanapokuwa na
wagonjwa wanaohitaji damu kutakiwa kununua damu hiyo.