GLADNESS MALLYA NA GABRIEL NG’OSHA
DAR ES SALAAM: Dunia ina mambo!
Mbuzi wanaosemwa kuwa ni wa ajabu, wanatikisa Jiji la Dar es Salaam,
baada ya kuonekana katika maeneo mbalimbali wakijichunga bila mwenyewe
kufahamika, lakini wakiwa hawaibiwi wala kubughudhiwa, Risasi
Mchanganyiko lina mkanda wa kusisimua.
Mbuzi hao wamekuwa wakijiongoza wenyewe,
wakila majani hadi kwenye matuta ya barabara zilizopo katika maeneo
mbalimbali ya jiji, jambo linalosababisha minong’ono na simulizi kadhaa
kwa watu. Jambo lingine linalowahusu mbuzi hao ni ukweli kuwa licha ya
kuonekana wako peke yao usiku na mchana, lakini hakuna mtu yeyote
anayewaiba, licha ya jiji hilo kuwa na idadi kubwa ya vibaka na wezi
pengine kuliko mikoa yote nchini.
“Mimi nilishuhudia watu wakiwapakia
mbuzi hawa usiku mwingi, nilijua kwa vyovyote hao ni wezi maana mwenyewe
hawezi kuja kuwachukua usiku, lakini sikujishughulisha nao kwa sababu
hata mmiliki halali simjui. Lakini asubuhi yake nilipopita nikawakuta,
nikapata hamu ya kujua kulikoni.
“Nilipoulizia, nikaambiwa eti wezi wale
walikwenda nao huko Kisarawe mkoani Pwani, lakini walipotaka kuwashusha
wakagoma, walitumia kila njia wakashindwa, wakaogopa na wakaamua
kuwarudisha, cha ajabu walipofika eneo lao tu, kabla hata hawajashushwa
walianza kuruka wenyewe kutoka kwenye gari,” alisema Emmanuel Juma wa
Tegeta.
Naye Zuwena Hamis mkazi wa Ubungo
alisema mbuzi hao wameshazoeleka, kwani wakati mwingine hutanda
barabarani kiasi cha kuyazuia magari maana mtu akiwagonga tu, lazima
apate ajali. “Ole wako umpige, utakiona cha moto, juzi walilala
barabarani magari yakashindwa kupita na kufanya madereva wageuze kwani
wanaho_ a ukimgonga mmojawapo hau_ ki Mkuranga,” alisema.
Gazeti hili lilimtafuta Msemaji wa
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Gaston Mwakyembe ili azungumzie
hatua zinazochukuliwa na jiji katika kuwadhibiti mbuzi hao kutokana na
uchafuzi wa mazingira, lakini simu yake ilirudisha ujumbe wa kuomba
udhuru, akiahidi kupiga muda mfupi ujao. Hata hivyo, alipotafutwa tena
baada ya saa mbili, simu hiyo haikupatikana kabisa.
SOURCE:GP