» » » Mimi ni mwanamuziki, Shilole ni mcheza shoo – Nuh Mziwanda

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Msanii wa muziki, Nuh Mziwanda ameendelea kumponda aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kwa kudai sio mwanamuziki bali ni mcheza shoo.

Muimbaji huyo wa wimbo ‘Jike Shupa’ amekuwa akitupiana maneno na Shilole kupitia mitandao ya kijamii toka wimbo huyo utoke.

Akiongea katika kipindi cha The Base kinachoruka katika runinga ya ITV, Nuh alisema hawezi shindana na Shilole kwa kuwa sio mwanamuziki.

“Mimi sitaki kiki, mimi mambo ya kiki nimeshayaacha, sasa hivi na fans base kwa ajili ya Jike Shupa,” alisema Nuh. “Ila yeye (Shilole) anajaribu kunichokonoa ili maisha yake yaende. Mimi ni mwanamuziki babu, siwezi kushindana naye, yule ni mcheza shoo,”

Shilole na Nuh hawakuachana vizuri, kila mmoja amekuwa akimtupia maneno machafu mwenzake.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post