ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
Tarime. Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga amewapa siku saba
wafanyabiashara wa Soko Kuu Tarime kurejea sokoni huku akiahidi
kushughulikia kero yao ya kutozwa ushuru mara mbili.
Luoga ameuagiza uongozi wa soko hilo kushughulikia na kumaliza
malalamiko ya wafanyabiashara kutozwa ushuru mara mbili kila siku
kinyume cha utaratibu.
Awali, mfanyabiashara Isack John alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa
wamelazimika kutoka nje ya soko kukwepa ushuru wanaotozwa na uongozi wa
soko ambao licha ya kulipa mara mbili, wanapewa stakabadhi moja pekee.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO