Dar es Salaam. Kama ulidhani lile sakata la ufukwe wa Coco Beach uliopo
kandokando mwa Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam linalomhusisha
Mwenyekiti wa Kampuni za Quality Group Limited (QGL), Yusuf Manji
limemalizika, elewa kwamba bado.
Manji amezungumza mambo mengi na gazeti la Mwananchi, lakini akasema bado anasubiria majibu yake kutoka kwa Rais John Magufuli baada ya kumwandikia barua Desemba, mwaka jana.
Mfanyabiashara huyo ambaye anatarajiwa kustaafu uongozi katika kampuni hiyo mwezi ujao, amesema anatamani kuona suala hilo linamalizika haraka.