Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania imemwagiza Mwanasheria Mkuu (AG)
kufanya maboresho katika Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA)
ndani ya miezi sita, ili kuzipatia mahakama za chini nguvu ya kusikiliza
makosa makubwa ya jinai na kuwaondolea wananchi kadhia ya kusota
rumande.
Agizo hilo lilitolewa na Mahakama hiyo katika hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Zephrine Galeba dhidi ya AG, aliyetaka Mahakama itamke kuwa vifungu namba 244 na 245 (1) (2) na (3) sura ya 20 iliyofanyiwa mabadiliko mwaka 2002, vinakinzana na ibara ya 13 (6) (a) ya Katiba ya mwaka 1977 inayotaka haki na usawa.
Katika kesi hiyo, mwanasheria aliyekuwa akimwakilisha Galeba, Wakili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk James Jesse aliiambia Mahakama kuwa kitendo cha makosa makubwa ya jinai kufunguliwa katika Mahakama zisizo na uwezo huo kinachelewesha haki.