» » Mama Kam, Milinga na Swevetta wapewa tuzo za Nyerere

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Dar es Salaam. Taasisi ya Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere imetoa tuzo kwa watu watatu walioonyesha kuziishi falsafa za Rais huyo wa kwanza wa Tanzania. Tuzo hizo zilizotolewa kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake miaka minane iliyopita, lengo likiwa ni kutunza na kuendeleza yote aliyosimamia Mwalimu Nyerere.
Tuzo hizo zilitolewa kwa Mwanzilishi wa Vikoba, George Swevetta, aliyekuwa Mkuu wa Sekondari ya Weruweru, Dk Maria Kamm na marehemu Mtimbanjao Milinga, aliyeanzisha vijiji vya ujamaa kabla Serikali kufanya hivyo.
Akiwaelezea washindi hao, mshereheshaji wa dhifa hiyo, Profesa Penina Mlama alisema ni jambo la heshima kuwa na watu wanaoweza kujitoa kwa ajili ya Watanzania kama alivyofanya Mwalimu Nyerere.
Swevetta alizianza harakati za kuwajengea uwezo kiuchumi watu wenye kipato cha chini hasa wanawake akiwa visiwani Zanzibar mwaka 2000. Baada ya miaka miwili, jitihada hizo zilizokuwa na mafanikio alizianzisha pia bara.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post