Monika akiwa amezimia.
Waandishi wetu, Amani
Dar es Salaam: Mapenzi uchizi!
Hii ndiyo kauli pekee unayoweza kuitumia baada ya mwanamke aliyetajwa
kwa jina moja la Monika, mkazi wa Tabata-Senene jijini Dar, kudaiwa
kumfumania mumewe na mchepuko ndani kwake kisha kuchoma moto nyumba
kabla ya kuzimia.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo
lililojaza umati, sekeseke hilo lilijiri wiki iliyopita, mishale ya saa
5:00 asubuhi nyumbani kwa wanandoa hao maeneo hayo ambapo mwanamke huyo
hakuwepo nyumbani hivyo aliporudi ndipo akaanzisha timbwili, akidai
kumkuta mumewe ndani na mchepuko.
“Monika aliangusha timbwili la aina yake lakini yule mchepuko alifanikiwa kutoka nduki.
“Tunashukuru Mungu, askari wa zima moto
walifika na kufanya jitihada za kumuokoa akiwa bado hajaungua la sivyo
sasa hivi tungekuwa tunazungumza mengine.
“Hata hivyo, Monika alitolewa ndani akiwa amepoteza fahamu,” alisimulia mmoja wa mashuhuda hao.
Amani lilifika
eneo la tukio na kuzungumza na majirani ambao walikiri kutokea kwa
mkasa huo ambao kwao ni wa kihistoria na kulaani kitendo hicho
kisijirudie mtaani kwao.
Ili kuweka sawa mzani wa habari hiyo,
gazeti hili lilizungumza na mwanaume huyo ambaye hakuwa tayari kutoa
ushirikiano kwa madai kuwa suala la kuchomewa moto nyumba yake lipo kwa
mwanasheria wake hivyo hawezi kulizungumzia.
Juhudi za kumpata mkewe ziligonga mwamba
lakini alipopatikana mjumbe wa eneo hilo, Joseph Salim alieleza namna
alivyosikitishwa na tukio hilo huku akiwalaumu mke na mume kutokana na
mwanamke kuchukua sheria mkononi na mwanaume kuingiza mchepuko nyumbani
anapoishi na mkewe.
Hata hivyo, kwa mujibu wa mjumbe huyo, tukio hilo halikufikishwa polisi kwa maelezo kuwa watamalizana wenyewe (mke na mume).
Waandishi: Mayasa Mariwata na Issa Mnally.
