Reli ndefu zaidi Afrika inayounganisha mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa na Dibouti yamalizwa kufanyiwa ujenzi.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la Ethiopia la ENA ni kuwa hafla maalum ya ufunguzi wa reli hiyo ilifanyika katika kituo cha treni jijini Nagad nchini Djibouti.
Rais wa Djibouti Ismail Omer Gulle na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn walikuwa miongoni mwa viongozi wakuu waliohudhuria sherehe hiyo.
Reli hiyo yatarajiwa kuboresha uhusiano wa kiuchumi baina ya mataifa ya kanda ya Mashariki mwa Afrika .
Takriban dola bilioni 3.4 ziligharibu mradi wa ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa kilomita 756.