Johann Ofner, 28, alipigwa risasi kifuani na kupoteza maisha pale pale.
“Wakati wa kutengeneza video ya muziki risasi kadhaa zilitumika. Hatujui majereha yalitokea vipi hadi sasa,” alisema Detective Inspector Tom Armitt. Ofner, anayefanya kazi kama stuntman, alikuwa akihusika kwenye video ya kundi la muziki wa hip hop la Sydney, Bliss n Eso.
Akiwa pia ni fundi seremala, Ofner amekuwa akifanya kazi kama stuntman kwa miaka kadhaa. Mwaka huu alikuwa ashiriki kwwenye shindano la TV, Australian Ninja.