» »Unlabelled » Mfanyabiashara Anaswa na mahindi ya bei chee kutoka nje ya nchi

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina moja la JAPHET amekamatwa na kikosi maalum  kinachohusisha TRA , POLISI na MAAFISA WA KILIMO akiwa anavusha mahidi kwa njia ya panya kutoka nchini Malawi bila ya kufuata utaratibu wa sheria.

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya saa 4:30 asubuhi, katika mpaka wa nchi ya Malawi na Tanzania wa Kasumulo Wilayani Kyela, kinyume na sheria za uingizaji chakula nchini.

Mahidi hayo yamekamatwa yakiwa kwenye gari moja aina ya Canter na mengine yalikuwa yamehifadhiwa kwenye 'store'.

Wakati wa uchukuaji wa mahidi 'store' kundi la wananchi walijitokeza na walianza kuwazuia maafisa wa TRA kupakia mahindi hayo kwa kile walichodai kuwa wanauziwa mahindi hayo kwa bei rahisi.

Kutokana na hali hiyo Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao na baadaye hali kurejea kuwa shwari

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limesema linaendelea na ufuatiliaji wa karibu ili kubaini wafanyabiashara wenye tabia kama hiyo.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post