Hatua hiyo ni baada ya wakali hao kwa muda tofauti kumuota rappa huyo na kuamini kuwa huenda alikuwa anawakumbusha kuwa wanapaswa kurudi kwenye muziki na kumuenzi kwa kufanya kazi ya pamoja.
Alianza rapa Noorah kwa kupost picha ya Albert Mangwea na kusema alimuota na jinsi alivyokuwa wakizungumza ni kama alikuwa hai na kitendo kilichomfanya Noorah atamani kuona ile ndoto kama ingekuwa ndiyo uhalisia lakini haikuweza kuwa kwa kuwa ni ndoto tu.
"Nimekuota usiku wa leo (jana) mshkaji wangu. Ilikuwa 'too realistic' kama vile bado upo hai. R.I.P ndugu yangu" aliandika Noorah
Baada ya hapo aliibuka Cpwaa na kudai hata yeye amemuota Albert Mangwea juzi hivyo ni kama rapa huyo anaongea nao, hivyo Cpwaa alimuomba Noorah warudi kwenye muziki kwani game ni kama imemiss sana ladha zao, hivyo Noorah alisema haina tatizo japo kwa muda huu bado anafanya matibabu kutokana na tatizo lake la kichwa, ila aliahidi kuwa atapita kwa Cpwaa ili wamalize kesi hiyo.
"Bro huwezi amini I did as well jana! Daah bro is talking to us. Come back my brother game ime miss ladha zetu Babastylz jana nime request sana ngoma za Ngwea kiwanja flani" alisema Cpwaa.