ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
Msafara wa kikosi cha Mamelodi Sundowns FC ya Afrika Kusini umewasili
leo Jumatatu mchana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuweka kambi kwa
muda kisha kucheza mechi mbili za kirafiki.
Mamelodi wamewasili Dar es Salaam wakiwa na jumlaya watu 42 huku ikielezwa kuwa wengine 10 wanatarajiwa kuingia kesho Jumanne.
Ikiwa Dar es Salaam, Mamelod inatarajiwa kucheza mechi za kirafiki dhidi
ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa kisha dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa
Azam Complex wiki hii kabla ya kuondoka Jumamosi ijayo.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO