Faki anachukua mahala pake Dlamini Zuma kutoka Afrika Kusini ambaye kipindi chake cha kuhudumu kimekamilika.
Mshindani ,mkuu wa bwana Faki katika duru ya mwisho ya upigaji kura, wakati wa kikao cha AU mjiji Addis Ababa, Ethiopia, alikuwa ni waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Kenya Amina Mohamed.
Wagombea watano waliokuwa wakiwania wadhifa huo ni pamoja na waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Kenya Amina Mohammed, mwanadiplomasia Abdoulaye Bathily kutoka Senegal, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Chad Moussa Faki Mahamat, mwanasiasa mkongwe kutoka Botswanda Pelonomi Venson-Moitoi na aliyekuwa wakati mmoja mshauri wa rais wa Equatorial Guinea Mba Mokuy.