» »Unlabelled » Tanzania inakuwa nchi ya kwanza kutunuku Astashahada ya uzamili ya uongozi wa forodha ya Afrika Mashariki

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Thursday, December 15, 2016

Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutunuku Astashahada ya uzamili ya uongozi wa forodha ya Afrika Mashariki, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuzinduliwa kwa mitaala ya Astashahada ya uzamili na stashahada ya uzamili katika uongozi wa forodha ya Afrika mashariki.

Jumla ya wahitimu 77 watatunukiwa Astashahada hiyo wote wakitoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika mahafali ya tisa ambayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa fedha na mipango, Dkt Philip Mpango.

Katika hatua nyingine TRA kupitia chuo cha kodi imeendela kubuni kozi mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya wadau ambapo jumuiya ya afrika mashariki imeanzisha mchakato wa kukitambua chuo hicho kuwa kituo cha umahiri cha Afrika Mashariki katika mafunzo ya forodha na kodi.

Katika mahafali ya tisa ya chuo cha kodi nchini, yatakayofanyika jijini Dar es salaam jumla ya wanafunzi 558 watatunukiwa vyeti, shahada na stashahada ambapo kati yao wahitimu wa kike ni 201 na wa kiume ni 357 .
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post