Thursday, December 15, 2016
Mkuu wa Mkoa Dsm Paul Makonda amekutana na wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga katika mitaa ya kariakoo na kutawaka kufanya biashara kwa kuzingatia Sheria na Utaratibu huku akiwaandalia utaratibu wa Kuwapatia shilingi million 100 kupitia chama chao ili kukuza biashara zao katika kiwango cha kati.
Akizungumza na wafanyabiashara hao ambao hivi sasa wameongezeka maradufu katika mitaa ya kariakoo na kusababisha adha na usumbufu kwa wapita njia,pamoja na kupanga bidhaa mbele ya maduka ya wafanyabiashara wengine amesema serikali iko katika mpango madhubuti wa kuhakikisha wanafanyabiashara katika mazingira mazuri na yenye tija katika maeneo yote ya jiji la Dsm.
Awali akizungumza katika soko la kariakoo baada ya kusikiliza malamiko yanayotokana na Upandishwaji kodi kwa wafanyabiashara kutoka 1700 hadi 3000 lakini pia wengine wakilipa shilingi elfu kumi kwa siku huku stakabadhi za malipo zinazotumika sio zile za mashine maalum ya EFD na kumtaamemtaka Mkurugenzi wa manispaa ya ilala kukaa pamoja na wanahisa ili kuchunguza malalamiko hayo ili hatua zichukuliwe dhidi ya watakaobainika kuhujumu mapato ya soko.
Aidha Makonda amesema soko madhumuni ya kuazishwa soko la kariakoo ni pamoja na uuzwaji wa mazo na bidhaa na zana za kilimo lakini hivi sasa limegeuzwa soko la kuuza vifaa vya viwandani huku mkuu wa soko hilo akikiri kuwa sheria zimekiukwa kutokana na changamoto ambazo hata hivyo alishindwa kuzifafanua alipotakiwa kutoa maelezo.