» »Unlabelled » Twite aeleza sababu za kuigomea Yanga

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

 Thursday, December 15, 2016

Dar es Salaam. Beki kiraka Mbuyu Twite ameeleza chanzo cha kugomea kushiriki kwenye mchezo ambao alidai Yanga ilimwandalia maalumu kwa ajili ya kumuaga dhidi ya JKU Jumamosi iliyopita.

Akizungumza na gazeti hili jana, Twite ambaye amemaliza mkataba wake Yanga tangu Novemba mwaka huu, alisema hakuona sababu ya kushiriki kwenye mechi hiyo.

“Yanga walinitaka niende kwenye mechi ile waliniambia ni maalumu kwa ajili ya kuniaga, kwanza niishukuru kwa kuona umuhimu wangu, lakini nilishindwa kwenda.

“Kwa mtizamo wangu niliona, mechi kama zile wanafanyiwa wachezaji wanaomaliza maisha yao ya soka na kuamua kupumzika, mimi sijaamua kupumzika, hivyo sikuona sababu ya kushiriki,” alisema Twite.

Akizungumzia hatima yake ya soka, Twite alisema ana mpango mbadala wa kwenda kutafuta maisha mengine ya soka nje ya nchi baada ya kutofikia makubaliano na timu kadhaa zilizoonyesha nia ya kumhitaji.

“Nimechelewa kuondoka kwa sababu ya pasipoti, natafuta nyingine kwani hii niliyonayo imejaa, kuna vitu vimesababisha ichelewe, lakini wakati wowote ikikamilika naondoka,” alisema.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post