Tuesday, December 13, 2016
Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako kusema waandishi waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi mwakani, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa msimamo wake dhidi ya kauli hiyo leo.
| Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Simon Sirro |
Kauli ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki tatu mfululizo akijibu yaliyoandikwa na vyombo vya habari kuhusu madai ya kulewa na kumfanyia fujo jirani yake.
Akizungumza na Mwananchi jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa sikukuu na atatoa ufafanuzi leo.