» »Unlabelled » Bei ya sembe, dona yaongeza ugumu wa maisha

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

 Tuesday, December 13, 2016

Dar es Salaam/ mikoani. Bei ya unga wa sembe katika mikoa mbalimbali nchini imepanda kutoka kati ya Sh800 na 1,000 kwa kilo hadi kufikia Sh1,500, huku mfuko wa kilo 25 ukiuzwa Sh29,500 badala ya kati ya Sh22,000 na Sh24,000.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Ruvuma, Tanga, Pwani na Lindi umebaini kuna ongezeko la bei ya unga kutokana na kuadimika kwa mahindi.

Mapema mwezi uliopita Mwananchi ilifanya uchunguzi wa mikoa maarufu kwa uzalishaji mahindi ya Ruvuma, Njombe, Mbeya na Rukwa na kubaini walanguzi walikuwa wakinunua mahindi na kuyasafirisha kwenda nchi jirani zenye uhaba wa chakula.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post