» »Unlabelled » Mwanamke ajifungua kwa kutumia tishu za ovari za utotoni

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Thursday, December 15, 2016

 Moaza asema atafurahi kuona wanawake wengi wasio na uwezo wa kuzaa wakisaidiwa kupata watoto kwa njia hiyo

Mwanamke aliyepata mtoto London kwa kutumia tishu za ovari zilizogandiswa akiwa mtoto ameelezea kuzaliwa kwa mtoto wake kama muujiza.

Inasemekana kuwa hii ni mara ya kwanza kwa madaktari popote ulimwenguni kutumia utaalam kama huo kuweza kupata mtoto.

Madaktari wake wanasema kuwa mafanikio hayo yatatoa matumaini zaidi kwa watoto wengine wenye tishu za ovari zilizohifadhiwa kabla ya kufanyiwa matibabu ya saratani.
 Mtoto wa Moaza alizaliwa katika hospitali ya London

Moaza Al Matrooshi,mwenye asili ya Dubai, alizaliwa na matatizo ya mfumo kwenye damu yaliyomfanya asiweze kuzaa akiwa mtu mzima ambapo tishu za ovari zake zilichukuliwa na kuhifadhiwa na wataalam hao wa afya ili kuchanganya na mayai yake atakapokuwa mkubwa kisha kupatikana kwa mtoto.
Tishu za ovari za Moaza zilivyochukuliwa na kuhifadhiwa

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post