» »Unlabelled » Mbeya City wafunguka na kusema Kagera Sugar lazima wakae

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

 Thursday, December 15, 2016


ZIKIWA zimebaki siku mbili kabla kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uongozi wa Mbeya City umesema kikosi chao kipo tayari kwa asilimia 100 na wapinzani wao wa Jumamosi, Kagera Sugar wajiandae kwa kipigo.

Meneja wa timu hiyo, Geofrey Katepa, akizungumza na gazeti hili jana, alisema benchi lao la ufundi limetumia vizuri siku 26 za mapumziko na kwa sasa wachezaji wake wapo tayari kwa mikikimikiki ya mzunguko wa pili.

Alisema kikosi hicho kilikuwa kwenye programu ngumu ya mazoezi kuhakikisha wanakuwa tayari kwa mzunguko wa pili unaoanza keshokutwa Jumamosi.

"Kwa asilimia zote vijana wapo tayari, tulikuwa na programu ngumu ya mazoezi na imemalizika, kwa sasa maandalizi ya kawaida yanaendelea," alisema Katepa.

Aidha, alisema mchezo wa wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar wataowaonyesha mashabiki mabadiliko makubwa yalivyo kwenye kikosi chao.

Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye mchezo huo wa keshokutwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mbeya City inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19 baada ya michezo 15 ya mzunguko wa kwanza.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post