» »Unlabelled » Malori ya Dangote yaweka historia Mtwara

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

 Monday, December 12, 2016

Mtwara. Shehena ya malori 651 kwa ajili ya kusafirisha saruji kutoka kiwanda cha bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote imeweka rekodi ya meli kubwa kuwahi kutia nanga katika Bandari ya Mtwara.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dk Khatibu Kazungu alisema kwa mara ya kwanza meli kubwa ijulikanayo Morning Composer imetia nanga na kushusha malori 651 katika bandari hiyo.

Akizungumza wakati wa mapokezi ya magari hayo bandarini hapo jana, Dk Kazungu alisema kufika kwa meli hiyo kutoka mashariki ya mbali kumefungua fursa za kiuchumi Mtwara na kuitangazia dunia kwamba bandari hiyo ina uwezo kama zilivyo nyingine duniani.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post