» »Unlabelled » Ligi ya soka DR Congo yasitishwa

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Thursday, December 15, 2016

TP Mazembe ndio mabingwa watetezi wa ligi DR Congo

Ligi ya kandanda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) imesitishwa kwa muda usiojulikana kutokana na sababu za kiusalama.

Serikali ililitaka shirikisho la soka nchini humo kusitisha mechi za ligi kuanzia Alhamisi.

Hatua hiyo imetokea huku wasiwasi ukiendelea kwamba huenda kukatokea vurugu muhula wa Rais Joseph Kabila utakapofikia kikomo wiki ijayo.

"Hali iliyopo nchini huenda ikafika viwanjani," Barthelemy Okito, katibu mkuu wa wizara ya michezo alisema.

Majuzi wakati wa mechi, mashabiki walisikika wakiimba kwamba muhula wa Kabila unamalizika.

Kabila alitakiwa kung'atuka 19 Desemba lakini amesema anapanga kusalia madarakani hadi Aprili 2018, wakati ambao serikali inasema itaweza kufanya uchaguzi ambao ulikuwa umepangiwa kufanyika mwezi jana.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post