» »Unlabelled » Maji ya kale zaidi duniani yagunduliwa Canada

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

 Thursday, December 15, 2016

 Maji hayo yaligunduliwa kilomita 3 chini ya ardhi kwenye mgodi Canada

Wanasayansi nchini Canada wamegundua maji yanayoaminika kuwa ya kale zaidi duniani, ambayo wanaamini yamekuwepo angalau kwa miaka bilioni mbili.

Maji hayo yamegunduliwa katika mgodi uliopo nchini Canada.

Wanasayansi walikuwa wamegundua maji mengine mwaka 2013 eneo hilo yaliyokadiriwa kuwa ya kutoka miaka 1.5 bilioni iliyopita lakini sasa wanasema maji waliyoyagundua karibuni ni ya zaidi ya miaka milioni mbili iliyopita.

Wanasayansi hao kutoka chuo kikuu cha Toronto waliwasilisha matokeo ya utafiti wao katika mkuano wa wataalamu wa fizikia ya dunia mjini San Francisco.

Profesa Barbara Sherwood Lollar, aliyeongoza wataalamu waliofanya ugunduzi huo aliambia BBC: "Watu wanapofikiria kuhusu maji haya, wanafikiri labda ni matono ya maji yaliyokwamba ndani ya jiwe.

"Lakini haya ni maji yanayotiririka. Yanatoka kwa kasi ya lita kadha kila dakika - ni maji mengi sana kuliko watu wanavyotarajia."

Maji ya awali yaliyoaminika kuwa ya kale zaidi yalipatikana 2.4km chini ya ardhi katika mgodi wa shaba nyekundu, zinki na fedha.

Wachunguzi waliendelea kufanya utafiti kadiri mgodi ulivyoendelea kuchimbwa.
Maji hayo yaliyogunduliwa sasa yalipatikana karibu 3km chini ya ardhi.
Mgodi huo unaendelea kuchimbwa

Maji hayo ya kale yanawapa wanasayansi fursa nadra ya kuchunguza historia ya sayari ya dunia, na pia kutoa vidokezo kuhusu viumbe walioishi wakati huo.

Watafiti hao wamegundua kemikali ambazo wanaamini zilitokana na viumbe wa seli moja ambao waliishi kwenye maji hayo.

Wanasema kuchunguza maeneo yenye maji kama hayo ya kale duniani kunaweza kuwadokezea iwapo kunaweza kuwa na uhai katika sayari nyingine katika Mgumo wa Jua.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post