» »Unlabelled » Mr Blue asema hahitaji meneja kwenye muziki wake, kisa?

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Msanii wa muziki wa kurap, Mr Blue amesema hahitaji kuwa na meneja wa kumsaidia katika kazi zake za muziki kwa kuwa tayari alishawahi kuwa na mameneja zaidi ya watatu ambao hawakumpatia mafanikio.Tokeo la picha la mr blue byser

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mboga Sana’ amesema alikuwa hawezi kuishi kwenye tasnia ya muziki bila kuwa na meneja lakini kutokana na kuona mchango wao kwake haukuzaa matunda.

“Mimi nilikuwa siwezi kuendesha maisha yangu ya muziki bila kuwa na meneja na nilifanya kazi chini ya mameneja watatu lakini kwa sasa nimesema basi sihitaji meneja tena nahitaji ushauri wa wadau namna ya kuboresha kazi zangu,” Mr Blue alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.

Rapa huyo pamoja na AliKiba wameshiriki kusapoti ngoma ya Abby Skills inayokwenda kwa jina la Averina , ambapo Abby amewataka mashabiki kumuunga mkono ili arejee vyema kwenye game kama zamani.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post