» »Unlabelled » Machinga Ilala, Dar ‘kiama’ chao leo

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema leo watafanya operesheni  ya kuwaondoa wafanyabiashara wadogo wanaopanga bidhaa zao kando ya barabara za Mabasi Yaendayo kwa Haraka  (Dart).
Tokeo la picha la maCHINGA ILALA

Operesheni hiyo itawahusu wote wanaofanya biashara eneo la Kariakoo Gerezani, Msimbazi, Ikulu kuelekea Soko la Feri na Shule ya Uhuru Mchanganyiko.

Mjema alisema wafanyabiashara hao wanatumia maeneo ambayo pia ni hatari kwa maisha yao kwa kuwa gari likikosea njia linaweza kuwagonga.

Alisema wengine kwa makusudi, huamua kutoa bidhaa zao sokoni na kuzipanga kando mwa barabara kwa madai ya kuwafuata wateja.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post